Advertisements

Tuesday, June 27, 2017

Bobi Wine akamatwa kwa kuingilia mkutano wa Rais Museveni


By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Mwanamuziki maarufu nchini Uganda, Bobi Wine amekamatwa leo, Jumanne na polisi kwa kukaidi amri ya kutofanya mkutano wa siasa katika eneo ambalo linakaribiana na mahali ambapo Rais wa nchi hiyo, Yoweri Musevenialitarajia kuhutubia.

Bobi Wine ambaye jina lake ni Robert Kyagulanyi, ni mgombea binafsi wa kiti cha ubunge katika jimbo la Kyadondo.

Imeelezwa kuwa Bobi Wine alizuiwa kufanya mkutano leo katika eneo la Kasangati kwa sababu lipokilomita chache kutoka eneo ambalo Rais Museveni alitarajia kufanya kampeni kumpigia debe mgombea ubunge wa chama chake cha NRM, Sitenda Sebalu.

Awali Bobi Wine alifikishwa Kituo cha Polisi cha Kisangati lakini alihamishwa baada ya wafuasi wake kuvamia eneo hilo wakitaka aachiwe mara moja.

Polisi walimwamishia Kituo Kikuu cha Kira lakini wafuasi wake walihamia kituoni hapo wakisisitiza aachiwe huru. Hata hivyo bado haijafahamika kama mwanamuziki huyo atashtakiwa.

No comments: