Advertisements

Tuesday, April 25, 2017

Polepole: Nape alikengeuka

Katibu wa Itikadi na Uenezi (KIU) wa CCM,
By Elias Msuya, Mwananchi emsuya@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekitaka chama hicho kumwajibisha Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kwa kauli yake kuwa alikitoa chama hicho shimoni.

Nape, ambaye alikuwa akishikilia nafasi ya Polepole kabla ya Uchaguzi Mkuu, alisema maneno hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Machi 23, siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Nape aliyetishiwa bastola kabla ya mkutano huo, alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

“Wamesahau wakati mimi nalala porini, wenyewe walikuwa wanakunywa bia baa. Nimekuwa mzalendo kwa nchi yangu, nimekuwa muungwana kwa chama changu na ninaapa kuwa muungwana kwa nchi yangu, hilo hakuna atakayelibadilisha. Lakini mimi nimekuwa mzalendo kwa CCM ambayo nimeikuta kwenye shimo inakwenda,” alisema Nape.

Lakini Polepole, ambaye jana alitembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayozalisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, alisema kama Nape alitoa kauli hiyo, alikuwa amekengeuka.

“Amekitoa Chama cha Mapinduzi shimoni? Kwamba, wakati anakitoa chama shimoni wengine walikuwa wanafanya nini?” alihoji Polepole.

1 comment:

Anonymous said...

Mimi ni mwanaCCM, na ni ukweli tulikuwa shimoni kiasi cha kwamba wengi tulihofu kuwa hatutashinda uchaguzi. Ndugu Polepole, acha mbwembwe, unataka Wana CCM tumwadhibu Nape kwa kusema ukweli? Kwani kusema ukweli ni dhambi? Wana CCM tuache huu mchezo wa kuwatisha au kuwazima wale wanachama ambao wanayo maoni au mtazamo tofauti. Demokrasia ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa chama chetu Uhuru wa kutoa maoni tofauti lazima uruhusiwe na kuheshimiwa. Hii hali ya uchochezi na vitisho ni hatari sana ndugu Polepole, utakiharibu chama chetu. Tunawahitaji watu kama Nape na vijana wengi ambao wanampenda ili wawe mstari wa mbele kukisaidia chama kipate tena ushindi hapo mwaka 2020. Kumbuka, ndugu Polepole, Nape aliishika hii nafasi yako, lakini hakuwa kijana mwenye vitisho au mentali ya udikteta na ndiyo maana vijana wengi bado wanamfuata hadi leo hii. Ni vyema kama utapungunza kutoa vitisho na kauli kali za mara kwa mara kwa wanaCCM wenzako na badala yake uige mfano wake Nape, kwa manufaa ya chama chetu.