Advertisements

Saturday, October 22, 2016

UZINDUZI WA TAARIFA YA HALI YA IDADI YA WATU DUNIANI

Mgeni Rasmi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (mwenye kaunda suti ya kijivu) akiwa katika Jukwaa Kuu na viongozi waandamizi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi kutoka Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA). Wengine pamoja nae ni Bw. Barnabas Yisa, Ofisa Mkaazi Mfawidhi UNFPA Tanzania (kushoto) na Mhe. Issa Juma Ally, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B (kulia).
Mhe. Salama Abuu Talib, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Zanzibar akihutubia wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Wananchi wa kijiji cha Kilombero, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatilia kwa makini yaliyokua yakijiri wakati hafla ya uzinduzi wa taarifa hiyo.
Bw. Barnabas Yisa, Ofisa Mkaazi Mfawidhi UNFPA (mwenye shati jeupe) akitoa neno kwa wananchi walioshiriki shughuli ya uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Idadi ya Watu Duniani. Kushoto ni Bibi. Christina Mwanukuzi Kwayu, Mwakilishi Msaidizi, UNFPA akitafsiri kwa lugha ya kiswahili hotuba ya Ofisa Mkaazi Mfawidhi.
 
Mhe. Issa Juma Ally, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, akitoa neno kwa wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Taarifa hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kuongea na wananchi na kuizindua rasmi.
Mgeni Rasmi Mhe. Thabit Kombo, Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akieleza juu ya fursa ndogo waliyonayo wasichana ya kumaliza skuli kuliko wavulana na wako katika hatari zaidi ya kukabiliwa na ndoa za utotoni, ajira za watoto, ukeketaji na matendo mengine ya udhalilishaji.
Wanafunzi kutoka shule za msingi katika kijiji cha Kilombero wakimsikiliza Mgeni Rasmi wakati akitoa hotuba kabla ya kuizindua Taarifa ya Hali ya Idadi ya Watu Duniani ambapo alisisitiza kuwa msichana wa miaka 10 anahitaji msaada mkubwa toka kwa familia, jamii na taifa, na kwa kumtimizia kikamilizfu haki zake anaweza kukua na kufikia hatma ile ambayo sote tunaitaka.
Mhe. Thabit Kombo, Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Taarifa ya Hali ya Idadi ya Watu Duniani.

No comments: