Advertisements

Monday, September 26, 2016

ASWIRA KUTOKA MKUTANO WA BARAZA KUU LA 71 LA UMOJA WA MATAIFA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa katika Mkutano wa Mawaziri wa Nje wa nchi za Jumuiya ya Madola.
Waziri Mahiga akibadilishana mawazo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sultanate of Oman, Bw. Yusuf bin Alawi bin Abdullah
Waziri katika Mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwaiti, Bw Sabah Al KHalid Ala Sabah
Waziri Mahiga alipoongoza kikao cha Troika ya SADC
Waziri Mahiga akibadilishana mawazo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sultanate of Oman, Bw. Yusuf bin Alawi bin Abdullah
Waziri alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Belgium Bw. Alexander De Croo

Na    Mwandishi  Maalum, New York
Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali,  kutoka   mataifa mbalimbali  duniani  kwa takribani wiki nzima iliyopita  wameendelea    kuelezea vipaumbele  vya nchi zao  mbele ya  wajumbe   wanaohudhuria Baraza Kuu la 71 la   UMoja wa Mataifa.
Mambo makubwa ambayo  karibu kila kiongozi ameyagusia katika  hotuba  yake ni  pamoja na  tatizo la kuongezeka kwa matukio ya  ugaidi,  tatizo la  wakimbizi na  wahamiaji, vita na machafuko vinavyoendelea katika nchi  kadhaa,  ubaguzi kwa misingi ya  dini au eneo analotoka mtu, mabadiliko ya tabia nchi na utekelezaji wa malengo mapya ya maendeleo endelevu.
Pamoja na viongozi hao  kushiriki katika majadiliano ya  jumla ya Baraza Kuu, lakini pia  wamekuwa  wakishiriki mikutano mingine ya pembezeni ambayo imeandaliwa sambamba na  mkutano mkuu.
Aidha   mikutano ya kimataifa na mikubwa kama huu wa 71 wa Baraza Kuu pia hutumika na viongozi  wakuu na  wa nchi na serikali kama  sehemu ya kukutana na kufanya mazungumzo  na kuweka mikakati ya  mahusiano baina  ya nchi zao.
Kama ilivyokuwa kwa Viongozi wengine, kiongozi wa ujumbe wa Tanzania   Dkt.Augustine Mahiga ( Mb) Waziri  wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa   Afrika Mashariki pia ametumia fursa ya  mkutano huu kukutana na viongozi wengine na kubadiliana mawazo na kujadiliana miongoni mwao  mambo  kadha wa kadhaa  yenye maslahi kwa pande zote mbili.
Yafuatayo ni baadhi  ya matukio  ambayo  Mhe. Waziri Mahiga ameshiriki    nje ya   majadiliano ya Jumla. Leo Jumatatu  Waziri  atapata fursa ya kuelezea  vipa umbele vya Tanzania wakati atakaposoma hotuba yake.

No comments: