Advertisements

Friday, July 1, 2016

SERIKALI YAWAONYA MABENKI NA MAKAMPUNI YA SIMU KUONGEZA TOZO KWA WATEJA ZAO

Serikali imezuia Benki kupandisha viwango vya tozo katika miamala yake na kuelekeza gharama hizo kwa wateja wao. 

Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata amesema kuwa asilimia 18 ya VAT mpya iliyopitishwa kwenye miamala ya benki inahusisha gharama zilizokuwa zikitozwa na benki hizo kwa wateja wao lakini serikali ilikuwa haipati chochote.

Kidata amesema kuwa Benki Kuu imeelekezwa kudhibiti benki hizo kwa kufanya ujanja wa kuongeza makato kwenye miamala ya wateja wao wakati wakijua fika kuwa hilo si lengo la kodi hiyo mpya.

Ameelekeza kuwa kiwango cha kodi kinachotozwa kwenye miamala hiyo kinatakiwa kubaki kama mwanzo lakini serikali itakata kodi yake ya asilimia 18 na kodi nyingine zilizopo kwa mujibu wa sheria

1 comment:

Anonymous said...

Shukran sana Serikali. They were getting rich at our expense and not paying Cesar's dues.