Advertisements

Thursday, June 30, 2016

YANGA NA SIMBA WAKISHINDANA KWA MANENO NA VIJEMBE TIMU YA BARCELONA INAONGEZA UKUBWA WA UWANJA WAKE, YANGA NA SIMA MMELOGWA AU UKILAZA WA VIONGOZI CHA CHAMA CHA MPIRA?

Yanga na Simba viongozi wenu hata awawezi kumka na kuacha marumbano yasiyo na mshiko na kutumia muda mwingi kushawishi makampunu yenye pesa kuwekeza kupitia time zenu kwa kupata japo uwanja wa mazoezi na gym. Kweli kazi hipo jitiririshi na hii habari ya kutoka huko Barcelona labda utashawishika.

Klabu ya Barcelona imeingia mkataba na kampuni ya Wapajapani ili kufanya marekebisho ya uwanja wake wa Nou Camp uwe na mwonekano mpya na kama hiyo haitoshi kuongeza idadi ya wanaoingia uwanjani kutoka watazamaji 90,000 waliokaa vitini hadi 105,000.

Kampuni ya Nikken Sennei Catalan inatarajia kuanza ujenzi huo mwaka 2017 kwa kitita cha pauni 465 na utamalizika mwaka 2021 lakini ujenzi utakuwa kwa awamu ili kuepusha kuathirika kwa ratiba ya mechi za nyumbani za Barcelona.

No comments: