Advertisements

Saturday, May 28, 2016

KIJANA ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUPANDA NA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU JIJINI MWANZA

Kijana Mmoja (pichani aliyeshikiliwa ) ambaye jina lake halikupatikana kwa haraka, mkazi wa Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati moja ya minara wa simu iliopo jijini humo, mchana wa leo.
Tukio hilo limetokea hii jana na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana.

Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia.
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Uokoaji na Zima Moto mkoani Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, ametoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa, ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati ya mnara huo.

Baada ya kijana huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure kwa ajili ya huduma ya kwanza. 

No comments: