Advertisements

Saturday, April 30, 2016

NICO NJOHOLE NA RENATUS NJOHOLE KUONGOZA SIMBA UGHAIBUNI, MPAMBANO WA WATANI WA JADI DALLAS, TEXAS LEO


Kikosi cha Yanga ughaibuni
Kikosi cha Simba ughaibuni
Renatusi Njohole akiwa katika picha ya Nico Njohole Dallas, Texas.

Wanandugu wawili Nicodemus Njohole na Renatus Njohole ambao kwenye nyakati tofauti waliwahi kuchezea timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi April 30, 2016 wataiongoza timu ya Simba ughaibuni kwenye mpambano wa watani wa jadi utakaofanyika jijini Dallas, Texas nchini Marekani.

Hii itakua ni mara ya nne kwa mpambano huu wa Simba na Yanga kuchezwa nje ya DC. Kama ilivyozoeleka watani hawa wa jadi mara nyingi mechi zao hufanyikia Washington, DC, na mara zote Yanga inaibuka mshindi.

Majimbo mengi ambako mpambano huu ulishawahi fanyika ni Columbus, Ohio, Chacago, Illinois na Houston, Texas.

Mpambano utakaochezwa Dallas katika kiwanja cha Hufthines Recreation Center ambacho anuani yake ni 200 N Piano Road, Richardson, TX 75081.unatarajiwa kuwa mkali kutokana na wachezaji wa Simba na Yanga kutambiana kila mtu akidai kuibuka na ushindi mnono.

Mapambano huu utakua wa wazi kwa mashabiki na wachezaji kujumuika pamoja na kuandika historia ambako kwa mara ya kwanza utaandika historia mpya ya kuchezwa na wachezaji wawili waliowahi kuichezea Club ya Simba. Michezo mingine iyakayokuwepo ni mpirsa wa kikapu na mpira wa wavu ikienda sambamba na nyama choma.

Mechi hii inayosubiliwa kwa hamu leo Jumamosi ni sehemu ya burudani itakayokuwepo kwenye kongamano la DICOTA ambalo mwaka huu limefanyika Dallas, Texas kuanzia April 28, mpaka kesho  May 1, 2016. 

Timu ya Simba ughaibuni ina historia nzuri inapocheza nje ya DC, mara zote imeibuka mshindi.

Mechi ya leo itakua ya tatu  kwa Simba na Yanga kugombea kombe la DICOTA mara ya kwanza timu hizi zilikutana kwenye kongamano la DICOTA lililofanyika Washington, DC mwaka 2011 na kongamano hilo Rais mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete ndiye aliyekua mgeni rasmi kwenye kongamano hilo..

No comments: