Advertisements

Friday, February 12, 2016

Waziri Mwigulu Nchemba Atumbua Jipu Machinjio Dar, Usiku




Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Lameck Nchemba alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye machinjio ya Ukonga, Mazizi jijini Dar, usiku wa kuamkia leo.
Waziri wa Kilimo na Mifugo Mwigulu Nchemba amefanya ziara ya Kushtukiza saa saba usikuwa kuamikia leo katika Machinjio ya Ukonga Mazizi.
Katika ziara hiyo, Waziri Nchemba amekamata ng’ombe 200 wakiwa wanaingizwa kwenye machinjio bila kibali halali, na kati yao ni ng’ombe 20 tu ndo walikuwa na kibali cha kuchinjwa, hivyo ushuru wa ng’ombe180 ulikuwa unatafunwa na watumishi waovu.
Baada ya kubaini hali hiyo,Waziri Nchemba ameufukuza uongozi wote wa machinjio hayo na kuagiza vyombo vya dola viwakamate viongozi wote waliohusika na kuwafikisha mahakamani.
CHANZO:GPL

No comments: