Advertisements

Saturday, October 10, 2015

TUJIKUMBUSHE TULIKOTOKA. JOHN BROWN MPIGANAJI KATIKA KUMALIZA UTUMWA, ALIEJULIKANA KATIKA SHAMBULIO LAKE LA HARPER FERRY 1859

Mwanaharakati John Brown alienyongwa mwaka December 2, 1859 huko west Virgina, ambayo ilikuwa ni sehemu ya state ya Virginia kwa wakati huo, jina lake halitasahaulika kwa harakati zake za kupigania kuondosha biashara ya utumwa.
Mji unaojulikana kama Charles Town ni mji iliopo west virginia ambayo zamani ilikuwa virginia wakati huo ambao alikamatwa na kuhukumiwa kunyongwa kwa mwa harakati aliekuwa akinga biashara ya utumwa  Bw. John Brown
Jefferson County Courthouse. Beginning on October 25, 1859, John Brown was tried in this courthouse built in 1836.

Juu ya balcon inatuonekana inaning'inia ni kama iliotumika kunyongewa Bw. John Brown huko Charles Town, ambayo imewekwa kumbukumbu mpaka leo katika mahakama ambayo ilimuhukumu adhabu hiyo ya kifo. PICHA NA KAMERA YA VIJIMAMBO ILIPOTEMBELEA WEST VIRGINIA

John brown alikuwa mwana harakati aliyekuwa akipinga biashara ya utmwa, amaye alizaliwa Mei 19, 1800 katika mji wa Torrington, Connesticut, kw a wazazi Ruth Mills na Owen Brown, ambayo ilikuwa familia kubwa iliyokuwa ikikabiliwa na matatizo kiasi Fulani ya kifedha katika maisha yake,. Owen aliamini utumwa sio sawa. Wakati akiwa na umri wa miaka kumi na mbili wakiwa safarini kupitia Michigan, alishuhudia mtoto wa kiume mwenye asili ya kiafrika akipigwa hii ilimsumbua kwa miaka na kumpelekea mwenyewe kuwa mwana harakati wa kukomesha uutmwa 

John Brown waliendesha harakari za chini kwa chini zijulikanazo kama (under groung railway) ya kutaka watumwa wawe huru, yeye aliamini katika kutumia nguvu kutamaliza utumwa, katika harakati hiyo, hatimaye uvamizi ulishindwa, alipelekwa mahakamani na alihukumiwa kifo na alinyongwa December 2, 1859 huko Charles town west virginia alikokamatiwa wakati huo ilikuwa Virginia 

Brown alifanya kazi za kujitolea kuhama hapa na pale kati ya miaka ya 1820 na 1850. 

Mwaka 1847 brown alikuta na msemaji mashughuri na mwana harakati huko springfield , massachusset na baadae mwa ka 1854 alihamia katika makaazi ya watu weusi huko kaskazini mwa Elba New York ambako kulitolewa ennea la ardhi kwa njia ya msaada na tajiri Gerrit Smith. 

Mwaka 1855 Brown alihamia Kansas, ambako pia watoto wake watano walihamia huko, Pamoja na kupitishwa kwa Sheria ya Kansas-Nebraska ya mwaka 1854, kulikuwa na mgogoro juu kama state itakuwa na hali ya kuwachia huru watumwa au hapana. Brown, ambao waliamini katika kutumia nguvu ili kumaliza utumwa, akawa kushiriki katika vita; katika 1856, yeye na watu wake kadhaa waliuwa walowezi wa tano wanaounga mkono utumwa katika shambulio kulipiza kisasi huko Pottawatomie Creek. 

Mwaka 1858 Brown aliwaachilia hour watumwa kutoka makaazi yao Missouri kuwaongoza kwenda Canada. Na brown aliongea kuwa na mpango wa kuunga jumuiya ya watu weusi huru katika milima ya Maryland na Virginia. 

Jioni October 16, 1859, brown aliongoza sehemu ya watu ishirini na moja kuvamia jeshi la serikali la Harpers Ferry Virginia ( amayo sasa ni west Virginia) waliwashikilia madarizeni ya watu katika mpango wa kupingana na utumwa. Vikosi vya brown viliendesha mapambano kwa siku mbili, hatimae walishindwa na vikosi vya kijeshi vikiongozwa na Robert E. Lee, watu wa Brown wengine waliuawa na wakiwemo watoto wawili wa brown na mwenyewe alikamatwa, kesi yake ilikwenda haraka na November 2, 1859 alihukumiwa kufa. 

Maelezo yake mahakamani kabla ya hukumu alieleza kuwa kitendo chake ni maagizo kutoka kwa Mungu, mjadala uliendelea kutaka mtazamo wa brown lazima uangaliwe. kuongezeka mgawanyiko kati ya Kaskazini na Kusini na kuwa na madhara makubwa kwa upande wa nchi. 

Baadhi ya wenzake pia walipinga kwamba mahakama inapaswa kuangalia hali ya akili ya Brown linapokuja suala la vitendo vyake. Brown aliuawa Desemba 2, 1859.

Tujikumbushe tulikotoka, itakuwa inawajia kila jumamosi na jumapili, tutakuwa tunaweka picha na video za matokeo mbali mbali yaliopita,(zamzni) ikwa mashuleni, kijijini, kazini, michezoni, maghafali mbali mbali, maigizo, nyimbo na picha binafsi. tafadhali tutumie kupitia email tujikumbushetulikotoka@gmail.com vikiambatana na maelezo, ili wasomaji na wadau wa vijimambo tuweze kujikumbusha mambo tuliopitia.



3 comments:

Anonymous said...

SIna uhakika kama tulikotoka ni kichwa sahihi cha habari hii.
Mimi nashauri iitwe tujikumbushe historia.
Mimi binafsi ni mtanzania na nilikotoka ni huko Tanzania.
Hii ni historia ya wamarekani na dunia kwa ujumla. Unakumbuka Triangular Trade? ndio mambo yenyewe hayo. Ila sio sisi tulikotoka

Anonymous said...

Kabisa huyo bwana licha ya yeye mwenyewe kuwa mtu mweupe lakini kihistoria aliyatolea maisha yake muhanga kuhakikisha kuwa watu weusi wanaondakana na mazila ya utumwa ingawaje suala hilo la kuwaachia watumwa kuwa huru liliendelea kuwaondoshea maisha kwa kila aliejaribu kuligusa hadi kupelekea vita vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa hivyo utaona mpaka hivi sasa kuna baadhi ya states za marekani bado bifu linafukuta kati ya watu weupe na weusi na la kushangaza zaidi sio watu weusi wenye bifu lakuwa kwanini walikuwa watumwa, hapana wenye kuendeleza bifu ni watu weupe kwanini mtu mweusi awe na haki sawa na mtu mweupe asibakie kuwa mtumwa tu?

Anonymous said...

MTOA MAONI WA KWANZA TULIKOTOKA INAONYESHA (SISI) NANI? WATANZANIA, LAKINI DHUMUNI NI KUJIKUMBUSHA IN GENERAL IN THIS WORLD, KWA KILA KITU NA KILA JAMII.
AHSANTE KWA MAONI