Advertisements

Saturday, October 10, 2015

MIKUTANO YA WB NA IMF YAZIDI KUVUTIA WENGI NCHINI PERU-LIMA



Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Wilson Masilingi akiwa na Mchumi mwambata Bw. Paul Mwafongo Kushoto pamoja na Afisa Mawasiliano Wizara ya Fedha Bi. Eva Valerian kulia wakiwa kwenye picha ya pamoja katika eneo la mikutano ya kimataifa ya Benki ya Dunia na shirika la fedha la kimataifa nchini Peru- Lima.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile wa pili kutoka kulia ( kwa nafasi ya uwaziri na Ugavana wa Benki ya Dunia) akiwa kwenye picha ya pamoja ya Mawaziri wa Fedha wa nchi 20 wanachama ( V20 - Vulnerable Twenty) watakao asirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi (climate change).Mawaziri hao wanatoka nchini Afghanistan, Bangladesh, Barbados, Bhutan, Costa Rica, Ethiopia, Ghana, Kenya, Kiribati, Madagascar, Maldives, Nepal, Philippines, Rwanda, Saint Lucia, Tanzania, Timor-Leste, Tuvalu, Vanuatu and Vietnam.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile aliyeweka kidole shavuni akiwa pamoja na ujumbe wa Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Fedha wakiwa katika ufunguzi wa mkutano wa kundi la nchi 20 zitakazo athirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi.


Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile wa pili kulia akitoa ufafanuzi kwenye majadiliano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop kushoto na Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu Bi. Mamta Murth kushoto kwake. Kutoka kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Wilson Masilingi, na baada ya katibu Mkuu kulia kwake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bi. Natujwa Mwamba.


Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu akitoa ufafanuzi katika majadiliano hayo pamoja na ujumbe wa Tanzania nchini Peru –Lima.


Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile wakiwa katika semina ya mafunzo ya namna ya kuzuia matumizi mabaya ya fedha.


Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa makini mafunzo ya namna ya kuzuia matumizi mabaya ya fedha.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akiteta jambo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Wilson Masilingi katika eneo la mikutano ya WB na IMF nchini Peru – Lima


Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Wilson Masilingi, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma pamoja na Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Bw. Said Magonya wakibadilishana mawazo baada ya kikao kilichokuwa na mafanikio hapa mjini Lima.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akifanyiwa mahojiano na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma kuhusu mwelekeo na mafanikio ya upatikanaji wa fedha za bajeti kutoka kwa wadau wa maendeleo hapa nchini Peru – Lima.

Katikati ni Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile akifurahia jambo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Wilson Masilingi (kulia) pamoja na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade (kushoto) wakifurahia jambo mara baada ya mkutano.


Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Wilson Masilingi, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Dr. Servacius Likwelile, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Wizara ya Fedha pamoja na Kamishna wa Fedha za nje Wizara ya Fedha Bw. Said Magonya akisoma ratiba ya mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa inayoendelea nchini Peru- Lima.


Baadhi ya ujumbe wa Tanzania wakijadiliana yaliyojiri kwenye mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa inayoendelea nchini Peru. Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Wilson Masilingi, Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade, Kamishna wa Fedha za nje Wizara ya Fedha Bw. Said Magonya na Mchumi Mwambata wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Paul Mwafongo.

Baadhi ya ujumbe wa Tanzania wakijadiliana yaliyojiri kwenye mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa inayoendelea nchini Peru. Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Wilson Masilingi, Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade, Kamishna wa Fedha za nje Wizara ya Fedha Bw. Said Magonya na Mchumi Mwambata wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Paul Mwafongo.
(Picha na Eva Valerian, Peru)

No comments: