Advertisements

Thursday, October 8, 2015

LOWASSA AFUNGA KAZI JIJINI ARUSHA LEO

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa akiwa ameambatana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mh. Godbress Lema, wakiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni, leo Oktoba 8, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, ARUSHA
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akihutubiwa wananchi, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, Jijini Arusha leo Oktoba 8, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mh. Godbress Lema, wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, Jijini Arusha leo Oktoba 8, 2015.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Arusha wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, Jijini Arusha leo Oktoba 8, 2015.
Mwanasiasa Mkongwe Nchini, Mzee Kingunge Ngomale Mwiru, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Arusha wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, Jijini Arusha leo Oktoba 8, 2015.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Arusha wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, Jijini Arusha leo Oktoba 8, 2015.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mh. James Mbatia, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Arusha wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, Jijini Arusha leo Oktoba 8, 2015.




















6 comments:

Anonymous said...

PENYE UKWELI UONGO HUJITENGA.HONGERA SANA WAKAZI WA ARUSHA KWA KUWAPA JIBU STAHIKI CCM.WANAHANGAIKA SANA CCM KWA MBINU CHAFU,PROPAGANDA MGANDO,MATUMIZI MAKUBWA SANA YA RUSHWA,YOTE HAYA KUJARIBU KUPUNGUZA MAKALI YA KIPIGO CHA PIMBI-MJINI HIYO JUMAPILI YA TAREHE 25 OCTOBA 2015 SIKU YA UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA.NI HIVI HAWANA JINSI CCM WATAKUWA WANAPOTEZA UDHIBITI WA NCHI KAMA CHAMA-DOLA BAADA YA KUWAPO MADARAKANI KWA MUDA WA MIAKA 55.WATANZANIA WALIO WENGI WANAENDELEA KUISHI KATIKA MAISHA DUNI,YA UFUKARA MKUBWA NA YASIYO NA MATUMAINI YA BAADAYE KWETU WANANCHI.AMETOKEA,AMEONEKANA MKOMBOZI WETU MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA,MTANZANIA MZALENDO MKAMILIFU,SHUJAA WA NYAKATI,MTANZANIA MAKINI MWENYE KUSUDIO LA DHATI LA KUINUA MAISHA YA WANANCHI,UCHUMI WA NCHI NA KUREJESHA NIDHAMU YA UTENDAJI SERIKALINI NA KWENYE TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA.ILI KUWEZA KUFUFUA ARI YA WANANCHI WENGI AMBAO WAMEKWISHA KATA TAMAA,MHESHIMIWA LOWASSA ANAZUNGUKWA NA TIMU IMARA SANA,KABAMBE YA WATENDAJI WENYE ARI KUBWA YA KUWATUMIKIA WATANZANIA,NA HILI NDILO TUNALO LIHITAJI ZAIDI WANANCHI.TAKWIMU MBALI MBALI ZINAONYESHA USHINDI WA MHESHIMIWA LOWASA UPO KATI YA ASILIMIA 78 HADI ASILIMIA 82.USHINDI WA LOWASSA HAUZUILIKI NA TUTASHUHUDIA KWA MARA YA KWANZA CCM KUFUTIKA KWA KUKOSA MBUNGE KATIKA MAJIMBO YA MKOA MZIMA AU KWA MAANA NYINGINE KIFO CHA GHAFLA CHA CCM MIKOANI NA KATIKA MEDANI ZA SIASA ZA NDANI NA NJE YA NCHI.KWA HERI CCM,JEHANAMU YA KISIASA NDICHO KITUO CHENU KIPYA,KWA HERI CM,MWENDE NA CHUKI ZENU,VIBURI VYENU,WIZI WENU,UHUNI WENU,UJAMBAZI WENU,UKUDA WENU.

Anonymous said...

Ndiyo nyumbani kwao, hata hivyo atamwaga pesa zake na kuwanunua wafuasi mpaka 25/10/15, hatimaye atajikuta hana kura za kushinda Urais>

Anonymous said...

Jazeni watu kibao kwenye kampeni zenu lakini mjue CCM ndani ya Ikulu tena 10/25/2015.

Anonymous said...

NILITEGEMEA KUPATA ANGALAU TEKE LA MWISHO LA MFA-MAJI WA CCM.ISINGEWEZEKANA SIFA KABAMBE NILZOWATOLEA WANANCHI WA ARUSHA TUKAKOSA KIRUSI WA CCM HATA MMOJA.MMEMSOMA UJINGA NA UPUUZI WAKE.HAO NDIO WALE TUNAOWAITA DIE-HARDS WA CCM WANAONA LAKINI KAMA HAWAONI,WANASIKIA LAKINI KAMA HAWASIKII.MWISHO NINA NENO.KWA SIKU ZILIZOBAKIA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU NITAKUWA INTENSE SANA KUWABOMOA CCM.NASIMAMA PEKE YANGU KWA CCM MILLION TATU HAWANIWEZI NINA KARAMA.NAWAOMBENI KIILA SIKU MPITIE MTANDAO HUU WA VIJIMAMBO,UNA HESHIMA KUBWA,NIMEUPENDA SANA,HAUBAGUI,HAUPENDELEI,YAANI NAJISIKIA FARAJA SANA.PIA KIILA SIKU FUNGUENI MTANDAO WA UDAKU SPECIALLY HAWA NAO NI PACHA NA HAWA VIJIMAMBO HUMO NAMO SIKOSI MPAKA TAREHE 24OCTOBA TUTAKAPOFUNGA KAZI JANGWANI.NAITWA NANJELE KIUNGANI KALINJELE AL-MAARUFU NIITE, NA-KIU.NDIYO,UPO HAPO MWANA-MABADIRIKO TANZANIA.

Anonymous said...

kweli watu wanaota ndoto za mchana. subiri sana ukawa washinde!!!!! ukawa ndio nini na ilani yao ni nini?? ninachoona ni wale mafisadii walikuwa ccm ndio wameenda huko kugombea. sasa subiri mle mandimu tarehe 27 oktoba majibu yakeshatoka.

Anonymous said...

si alikuwa arusha na Kilimanjaro wiki iliyopita!! sasa ameona magufuli kajaza na yeye presha imemuingia karudi tena, utarudii sana wananchi wanakula pesa zako na kura hawakupi. nani akuchague wewe kwa sifa gani uliyokuwa nayo zaidi ya kununua chama cha chadema.