Advertisements

Saturday, October 10, 2015

LOWASA AAHIDI NEEMA KWA WAKULIMA WA ZAO LA KAHAWA KILIMANJARO

Kada mkongwe wa Chama cha Mapinduzi,aliyejiengua hivi karibuni ,Kingunge Ngombalemwiru akisalimia wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea Urais kupitia Chadema na Vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA uliofanyika katika viwanja vya mashujaa mjini Moshi.Picha zote na Dixon Busagaga wa Busagaga's Orijino Blog.
Kada mkongwe wa Chama cha Mapinduzi,aliyejiengua hivi karibuni ,Kingunge Ngombalemwiru akimkaribisha mgombea Urais kupitia Chadema na Vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA ,Edward Lowasa kuzungumza na wakazi wa mji wa Moshi katika viwanja vya Mashujaa mjini Moshi.
Mgombea Urais kupitia Chadema chini ya mwavuli wa vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ,Edward Lowasa akizungumza na maelfu ya wakazi wa mji wa Moshi na Vitongoji vyake waliofika kumsikiliza katika mkutano uliofanyika viwanja vya Mashujaa mjini hapa.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ,(Chadema) taifa ,Freeman Mbowe akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa Mjini Moshi.

Maelefu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni wa mgombea Urais kutia Chadema kwa mwavuli wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA,wakionesha ishara ya mabadiliko.
Mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi,UKAWA,James Mbatia akizungumza katika mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea Urais ,Edward Lowasa uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi.

Mwenyekiti Mwenza wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA,James Mbatia akiwa amemnyanyua mkono na kumuombea kura mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael
Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael (Chadema) akizungumza na maelefu ya wananchi waliofurika katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi katika mkutan wa kampeni wa kumnadi mgombea Urais kupitia UKAWA,Edward Lowasa.

6 comments:

Anonymous said...

hiyo ndiyo UKAWA bwana.

Anonymous said...

Basi kama mtu unampiganaji wako sasa ukianza kumuona anadifendi baada ya kushamblia ujuwe utapoteza tu mpambano. Magufuli alikuwepo Arusha baada ya kuondoka tu lowasa kaenda kudifendi baada ya kuuza sera zake. Vilevile magufuli alikuwepo karatu na Kilimanjaro baada ya kuondoka tu lowasa karudi kudifendi hakuna anachokifanya isipokuwa poor defending sasa kwanini CCM isishinde kirahisi, alafu wanakuja kalalamika wamefungwa goli la mkono? Kwa sababu CCM hawataacha mashambulizi mpaka dakika za nyongeza, CCM wanawashambuliaji wengi kukaa kusubiri mashambulizi ya magufuli huku wakati ukipotea bila ya kuweka tafakari ya washambuliaji wake wa pembeni watakuwa wanazunguka around the clock kwa kweli timu ya ushindi si ile inayosubiri kudifendi muda wote.

Anonymous said...

Wewe mchangiaji namba mbili hapo juu usibwabwaje kama mtu ambaye hajaenda shule. Ratiba ya mikutano ya kampeni ilipitsihwa na kutangazwa na Tume ya Uchaguzi tangu mwanzo wa kampeni, hakuna mtu anajiendea tu kwa ratiba yake au kwa hulka zake kama unavyodhania. Ndiyo maana Mkapa anawita Watanzania Malofa na bado wanashangilia na kuimba nyimbo za CCM. Ukiona wazee kama Kingunge ambaye amekuwemo ndani ya chungu kwa zaidi ya miaka 60 anakimbia basi ujuwe huko ndani kuna moto mkali. Subirini mtaona baada ya Oktoba 25,Tanzania will not be the same again!!

Anonymous said...

Wewe Anonymous wa 6:22 AM. Umebakisha 2 weeks mtaji wako wa buku zako saba kumalizika. Kambaree wewe

Anonymous said...

Umekosa cha kusema. Ati kudifendi!! shule ulifikia wapi? Okay elimu hewa ya ccm. Pole sana Lowasa ndiye Rais

Anonymous said...

Mnakaribishwa Ikulu baada ya kupiga kura hapo tarehe 25/10/2015 kwenda kuhudhulia sherehe ya kuapishwa Magufuli kama rais wa tano wa Jamhuri wa Muungano.