Advertisements

Saturday, October 10, 2015

JK AUMWAGIA SIFA MFUKO WA PENSHENI WA PPF KWA UWEKEZAJI BORA

 
RAIS Jakaya Kikwete, akitoa hotuba kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi la kitegauchumi PPF Plaza eneo la Vigaeni, mjini Mtwara, Oktoba 10, 2015. Jengo hilo la ghorofa  mali ya PPF litagharimu shilingi Bilioni 9.5 ujenzi wake utakapokamilika mwishoni mwa mwaka huu. 

NA K-VIS MEDIA, MTWARA

RAIS Jakaya Kikwete ameumwagia sifa kemkem Mfuko wa Pensehni wa PPF, kwa uwekezaji bora, wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jingo la ghrorofatano  la kitegauchumi la PPF Plaza mjini Mtwara Oktoba 10, 2015.
“Nimefurahishwa sana na uwekezaji wenu kwani ninaenda kustaafu na kupumzika kwa raha kutokana na mambo makubwa mliyotafanya, nah ii ni fursa nzuri kwa uwekezaji kwenye mkoa huu ambao utakuwa kitovu cha uchumi.” Alifafanua Rais.
Rais Kikwete, ambaye alitua mkoani humo akitokea nchi I Msumbiji alikokwenda kuaga, alisema, Mtwara yuko muwekezaji ambaye ni tajiri mkubwa barani Afrika akishikilia namba moja, nay eye angependa walau kulala mkoani Mtwara wakati wa ziara zake za kukagua miradi yake, na lakini atalala wapi, wakati hakuna hoteli yenye hadhi yake.? Aliuliza na kuwataka wawekezaji zaidi katika eneo la mahoteli ili kuweza kuwapokea wafanyabiashara wakubwa wanaotembelea Mtwara ivi sasa.
Akitoa taarifa ya ujenzi huo, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Aggrey Mlimuka, alisema, jingo hilo litakapokamilika ujenzi wake litagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 9.5 na tayari baadhi ya ghorofa zimeshachukuliwa.

 Rais Jakaya Kikwete, (katikati), akipunga mkono kuwaaga wafanyakazi wa PPF na wajenzi wa jingo la kitegauchumi la Mfuko huo “PPF PLAZA” baada ya kuweka jiwe la msingi
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Subira Athumani, mfano wa kadi ya uanachama kupitia mpango wa “Wote Scheme” ambao unahusu kujiunga na uanachama kwa uchangiaji wa hiari. (Kushoto), ni Naibu waziri wa fedha, Adam Malima, na wapili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, Aggrey Mlimuka


Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, akitoa hotuba kumkaribisha Rais Kikwete kuweka jiwe la msingi la jingo la kitegauchumi la PPF mjini Mtwara Oktoba 10, 2015
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Aggrey Mlimuka, akitoa hotuba wakati wa uwekaji jiwe la msingi la jingo la kitegauchumi la Mfuko huo mjini Mtwara Oktoba 10, 2015


 Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Aggrey Mlimuka, wakiwa katika picha ya pamoja na Mwanachama mpya wa mpango wa uchagiaji wa hiari (Wote Scheme), wa Mfuko huo, Subira Athumani Makumbiri, baada ya kukabidhiwa mfano wa kadi ya uanachama
Ngoma za utamaduni nazo zilikuwepo kunogesha shughuli
 Baadhi ya wafanyakazi wa PPF, na wajenzi, waimpungia mkono Rais na ujumbe wake wakati waiondoka eneo la tukio
 Wajumbe wa bodi ya wadhamini ya PPF, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Aggrey Mlimuka, (wane kulia), na wafanyakazi wa PPF, wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, ambaye pia ni Mkurugenzi wa uwekezaji, Steven Alfred (wakwanza kushoto mstari wa mbele)
 
Rais Jakaya Kikwete, (kushoto), akiangalia ushuhuda uliokuwa ukitolewa na Mwanachama wa PPF kupitia mpango wa Wote Scheme, baada ya kuweka jiwe la msingi la kitegauchumi la Mfuko huo mjini Mtwara Oktoba 10, 2015. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, Aggrey Mlimuka, Wakwanza kulia ni Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngoi, na Meenja Uhusiano Lulu Mengele
 Rais Kikwete, na Mama Salma Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na naibu waziri wa fedha, Adam Malima, Waziri wa Nishati, George Simbachawene, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, Wajumbe wa bodi ya wadhamini ya PPF, Wafanyakazi wa PPF, na wajenzi wa jingo la kitegauchumi la PPF Plaza mjini Mtwara leo Oktoba 10, 2015. (Picha zote na K-VIS MEDIA/Khalfan Sad)
 Rais Jakaya Kikwete, (katikati), akiteta jambo na Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Pensheni wa PPF, Aggrey Mlimuka, wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwenye jingo la kitegauchumi la Mfuko huo, PPF Plaza mjini Mtwara
 Rais akisalimiana na mmoja wa wajumbe a bodi ya wadhamini ya PPF, Bi. Amelye
 Rais akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa uwekezaji, Steven Alfred
 
Kaimu Mkurugezi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Steven Alfred, akitoa hotuba wakati wa uwekaji jiwe la msingi la jingo la kitegauchumi la Mfuko huo mjini Mtwara Oktoba 10, 2015
Jengo la kitegauchumi la ghorofa 5 linalomilikiwa na Mfuko wa Pensehni wa PPF, eneo la Vigaeni mkoani Mtwara, ambalo Rais Jakaya Kikwete, ameliwekea jiwe la msingi leo Oktoba 10, 2015

No comments: