Advertisements

Tuesday, August 4, 2015

NENO UKABILA LATAWALA KAMPENI ZA CCM KURA ZA MAONI JIJINI MBEYA

Na Mwandishi wetu,Mbeya 
BAADHI ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya, wamekitaka chama cha mapinduzi, kutoa onyo kali kwa wanachama wake ambao ni miongoni mwa wagombea nafasi ya ubunge Jimbo la Mbeya mjini, kuacha kutoa matamshi yanayoashiria vitendo vya ubaguzi wa kikabila.
Wakizungumza jiji Mbeya , mara baada ya chama hicho kupitia wilaya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa ubunge kwa  wagombea 16 ambao walijitokeza kuwania nafasi hiyo.
Walisema, chama kama chama hakijaundwa wala kuongozwa na sera ya ubaguzi wa aina yoyote ile hivyo wanashangazwa na matamshi ya ubaguzi yanayotolewa na baadhi ya wagombea hao.
“Hivi leo chama kimefikia hatua ya kuwakumbatia watu ambao wanaeneza sera ya ukabila hii ni hatari kwa Taifa letu kwani ni uchochezi na ukiachwa utaliangamiza taifa hili,”alisema God Julius mkazi wa majengo ambaye pia ni mwanachama wa chama cha mapinduzi.
Alisema, kunahatari ya kukipoteza chama kwa makosa madogo ambayo yamekuwa yakifumbiwa macho na viongozi na wakati mwingine kufanywa na viongozi hao.
“Leo mwanachama wa ccm anasimama na kusema jimbo haliwezi kuongozwa na mtu ambaye si mzawa na kumfafanisha mtu huyo sawa na kibaka, hilo ni tendo  la aibu na si uungwana wakati umefika kwa chama kuchukua hatua,”alisema.
Alisema, CCM ni sawa na taasisi kwani imeundwa kwa kufuata miongozo na kuongozwa kwa taratibu na sheria na ikumbukwe kwamba chama kimebaba watu tofauti tofauti na makabila tofauti hivyo watu wakianza kubaguana kwa ukabila ni ishara mbaya ambayo inaweza sababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
“Katiba na sera ya CCM inaeleza kwamba kila mtu mbaye ni mtanzania anahaki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hivyo, tukianza kubaguana hii ni hatari,”alisema Mwajabu jamari mkazi wa Soweto.
Alisema, wagombea wanasimama kwenye umati wa watu na kushangilia huku wakitoa kauli za chuki kwa wagombea ambao si wazawa ni vema chama kikachukua hatua za kinidhamu.
Hata hivyo, aliwatahadharisha wagombea hao kwamba wakumbuke familia zao zinaishi kwenye mikoa mbalimbali hivyo na wao wakibaguliwa wasishangae.

Mwisho.

No comments: