Advertisements

Saturday, July 25, 2015

Lowasa kutangaza kuhamia CHADEMA Julai 26, Mwembe yanga ambako Dr Slaa alimtangaza kuwa Fisadi Papa...KAZI IPO!!


Zipo taarifa za uhakika kwamba Edward Lowasa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa Richmond anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari Jumapili tarehe 26 Julai 2015 Jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo, Lowasa anatarajiwa kueleza mambo mengi juu ya mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM uliopelekea jina lake kukatwa.
Pia katika mkutano huo, Lowasa anatarajiwa kutangaza rasmi kujivua uanachama wake ndani ya CCM na kujiunga na CHADEMA ambapo baadaye jioni ataelekea viwanja vya Mwembeyanga ambako ataungana na viongozi wengine wa CHADEMA kwenye mkutano wa hadharaza. Mtakumbuka kuwa uwanja huo wa Mwembeyanga uliopo Temeke Dar es Salaam ulitumika kutaja orodha ya mafisadi 11 na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Wilbroad Slaa mwaka 2007 ambapo jina la Lowasa lilikuwa miongoni mwa majina yaliyopo kwenye orodha hiyo.

Uamuzi wa Lowasa kwenda CHADEMA umetokana na kutimiza makubaliano ya kupeleka shilingi bilioni 10 ambapo fedha hizo zimekabidhiwa Jana Alhamis Tarehe 23 Julai 2015. Aliyekabidhi fedha hizo kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ni Apson Mwang'onda na makabidhiano yamefanyika kwenye Hotel ya Sea Cliff huku tukio hilo likishuhudiwa na Kingunge Ngombale Mwiru na wengine ambao sitawataja kutokana na sababu maalum.

Taarifa zinasema kuwa kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa watu walioathirika na kukatwa kwa Lowasa hasa kutokana na fedha nyingi na muda kwa matumaini kuwa watakuwa "UPPER" baada ya Lowasa kushinda Urais. Miongoni mwao ni pamoja na Prof Juma Kapuya, Nazir Karamagi, Parseko Kone, Mgana Msindai, Kingunge Ngombale Mwiru, Mchungaji Gwajima, Andrew Chenge nk.
Hata hivyo, inadaiwa pia kuwa watu walio karibu na Lowasa akiwemo mfadhili wake mkuu Rostam Aziz ambaye amegoma kutoa fedha za kufadhili harakati za kwenda upinzani wanaendelea kumsihi kuwa asiende huko kwani atakuwa amejimaliza kabisa kisiasa. Pia inadaiwa kuwa mkewe Regina Lowasa amekuwa bitter sana na mpango wa mumewe kwenda upinzani na kwamba kwa siku kadhaa sasa amekuwa akiwafukuza wageni waliokuwa wanaenda nyumbani kwake hasa wale wa upinzani.
Credit:Thechoice.com

3 comments:

Anonymous said...

Kupokea fedha ili uhamie chama kingine?is it?kama ni kweli,basi mh hukuwa na nia nzuri ya kuomba uraisi,ila ulikuwa na nia nyingine!kamati kuu ilionambali kumchagua magufuli kuongoza nchi yetu.why do that mh?y?y?hakika kama ni kweli utakuwa hujawatendea haki wanaokuamini mh!nafasi si uraisi tu hata ubunge na michango yako bungeni tunahitaji sana toka kwako.why take that money!no!no!no!please dont do that!

Anonymous said...

Tanzania inatakiwa kuamka sasa. Mh. Lowassa sidhani kama ana makosa makubwa zaidi ya waliokula fedha ya escrow hadi hata viongozi wa kidini. Lazima waTanzania tukue na wakati kwani hatutakiwi kuwa hapa tulipo na yote ni kutokana na viongozi wa serikali inayoongoza. Ukweli ubakie kuw aTanzania inahitaji mabadiliko. haya maswala ya kupata kupitia goli la mkono sio sahihi. Kuna mbinu nyingi tu zimekuwa zinatumika katika daftari la kuandika wapiga kura na yote haya ni njama za serikali tume yenyewe kwa kutaka kuendelea kuwepo madarakani!!

Anonymous said...

Uchungu wa mwana aujua Lowassa. Hata waseme nini Baba Lowassa nenda tu liwalo na liwe hata KANU ya Kenya walijiona vijimiungu watu kama ccm na wakazikwa. Zika hicho chama kabisa. Mwandishi wa habari hii ni ccm kamili. Umeandika hii habari kwa machungu makubwa inavyosomeka. Haijalishi yote ni siasa tu. Tunajua siasa is just a game. Kama walimchafua watamsafisha. Walikuwa bado hawajajua ukweli ila sasa wanajua Lowassa ni safi.