Advertisements

Friday, May 29, 2015

Kwa mara ya kwanza tangu atoke jela, Francis Cheka apima uzito kuzichapa na Mthailand kesho!


BONDIA Francis Cheka wa Tanzania na Kiatchai Singwancha kutoka Thailand wamepima uzito leo kwenye ukumbi wa Green Grill uliopo maeneo ya Victoria jijini Dar es Salaam tayari kwa pambano lao linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Masumbwi.
Pambano hilo litapigwa kesho usiku kwenye ukumbi wa PTA Manispaa ya Temeke.

Cheka na Singwancha watazichapa kwenye pambano hilo la raundi 10 lisilo na ubingwa wowote, lakini ni mabondia hao wawili wanatafuta kulinda heshima. 

Singwancha alitua Dar jana akiongozana na kocha wake tayari kwa ajili ya pigano hilo ambalo linatarajiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na historia ya mabondia wote wawili.

Pambano hilo ambalo litakuwa ni la kwanza kwa Francis Cheka toka atoke jela linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa ndondi nchini ili kuona kama ataweza kumsambaratisha Mthailand huyo ambaye ana rekodi nzuri ya kupiga kwa Technical Knockout (KO).

Cheka amesema kuwa, anataka kuudhihirishia umma wa Tanzania kuwa bado yuko vizuri kwenye makonde na ili kuthibtisha hilo atashinda pambano lake kesho, lakini akawaomba wapenzi, mashabiki na wadau wa mchezo wa ngumi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumuunga mkono ili amsambaratishe mpinzani wake.

“Jela ni jela na ngumi ni ngumi, hakuna chochote kutoka jela kilichoathiri uwezo wangu wa kupambana ulingoni,watanzania wajitokeze tu kuja ‘kunisapoti’ ili nimchape mthailand. Wengi wanaujua uwezo wangu sitai kuzungumza mengi kwenye hilo”, amesema Cheka.

“Ninauhakika wa kushinda kwasababu mimi najua ngumi, ukiwa unajua kitu unakuwa na uhakika na unachokifanya, kwahiyo watanzania watarajie ushindi kutoka kwangu”,aliongeza Cheka.

Kwa upande wake Singwancha ametamba kuwa, atashinda kwa kumpiga Cheka licha ya kukiri kutofahamu uwezo wa bondia huyo ambaye kwa sasa anatamba kwenye masumbwi hapa Tanzania.

“Sifahamu chochote kuhusu Francis Cheka zaidi ya kusikia jina lake, sijawahi kumuona akiwa ulingoni. Hilo halinitishi wala kunipa wasiwasi kwasababunimejiandaa vizuri na ninauhakika wa kushinda pambano hilo la kesho. Nimefanya mazoezi ya kutosha chini ya kocha wangu na nipo katika hali nzuri kwa ajili ya kesho”, Singwanchi amesema.

Takwimu za mabondia hao

Francis Cheka

Global ID: 185091

Sex: Male

Birth date: 15 April 1982

Division: Super middle weight

Heght 5’10.5”/ 179 cm

Current weight: 75.7 Kg

Country: Tanzania

Won 30 (KO 16)+Lost 8 (KO 5)+Drawn 2=40

Kiatchai Singwancha

Global ID: 67387

Sex: Male

Birth date: 17 October 1982

Stance: Southpaw

Heght 5’ 7”/ 171cm

Current weight: 75 Kg

Country: Thailand 



Won 35 (KO 24)+Lost 12 (KO 9)+Drawn 0=17
Credit:Shaffihdauda

No comments: