Advertisements

Friday, May 29, 2015

Buhari ameapishwa kuwa rais wa Nigeria

Buhari ameapishwa kuwa rais wa Nigeria

Mshindi wa uchaguzi mkuu nchini Nigeria Muhamadu Buhari ameapishwa kama rais mpya wa nchi hiyo.
Waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani akiwa Abuja

Bwana Buhari ambaye ni kiongozi wa zamani wa kijeshi amechukua uongozi kutoka kwa rais wa zamani Goodluck Jonathan ambaye amemtaka kuiunganisha nchi hiyo wakati inapokabiliana na tisho kutoka kundi la Boko Haram.Kiongozi wa Ethiopia akiwasili Abuja

Buhari anasema kuwa lengo lake ni kupambana ufisadi ambao umekita mizizi katika taifa hilo lenye watu wengie zaidi barabi Afrika.Wasanii wakiwatumbuiza wageni

maelfu ya mashabiki na wafuasi wake walishangilia Jenerali huyo mtaafu alipokula kiapo cha kulinda nchi hiyo.Waandishi wa habari

Hii ndiyo mara ya kwanza kwa kiongozi wa upinzani kumshinda rais aliyeko madarakani.

Viongozi kutoka mataifa mengi duniani wakiongozwa na waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John kerry , rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma miongoni mwa wengine wengi.Rais Buhari akikagua guaride la heshima

Muhammadu Buhari, ni Muisilamu, mzaliwa wa Jimbo la Katsina, Nigeria kaskazini.

Alizaliwa mwaka 1942, Buhari alikuwa kiongozi wa saba wa taifa la Nigeria, baina ya mwaka 1983-1985.Msanii akinasa kumbukumbu ya leo

Ni jenerali mstaafu aliyepata mafunzo ya kijeshi katika Nigeria, Uingereza, India, na Marekani.

Na aliwahi pia kushika nyadhifa za ugavana, kamishna wa raslimali ya mafuta, mwenyekiti wa shirika la umma la mafuta, na pia mwenyekiti wa Mfuko wa Amana ya Mafuta.Familia ya rais Buhari

Anasemekana kuwa si m-kaishi, hakubali kushindwa.

Licha ya kushindwa mara katika chaguzi tatu, amerejea kushindania tena urais, dhidi ya rais alo-madarakani Goodluck Jonathan,Maafisa wa kijeshi

Mkristo, anaye toka eneo la Niger Delta, kusini Nigeria, kwa mara ya pili, katika uchaguzi wa Machi. Unaonesha kuwa mchuano mkali.

Kuambatana na mandhari ya kisiasa, Buhari si limbukeni. Kushindwa mwaka 2003 na tena 2007, alitambia matokeo ya chaguzi hizo mahakamani bila mafanikio.Waageni waalikwa

Ingawaje, Buhari anazingatiwa kuwa kiongozi mwenye ufuasi mkubwa na heshima nyumbani, hususan katika rubaa za kaskazini Nigeria.

Na hii inatokana na sera zake za kupambana na ufisadi na ukosefu wa nidhamu, wakati alipokuwa mtawala wa kijeshi.Awali wageni walilazimika kupiga foleni kubwa kabla ya kuingia uwanjani

Kimataifa, Buhari pia anasemekana kuheshimiwa.

Yajulikana kwamba ni yeye na marehemu Nelson Mandela tu ndio Wafrika binafsi waloalikwa na Ikulu ya White House, Marekani, kuhudhuria sherehe za kutawazwa Barack Obama.

Kampeni ya Jenerali Buhari, ilitilia mkazo mambo kadha, miongoni mwake utawala bora, kufufua uchumi, maendeleo ya miundombinu,

umeme na nishati, kilimo, elimu, afya, ardhi na usafiri, kuwezeshwa wanawake, usalama, na ajira. Ingawaje, uwili wa nafsi yake bado unazusha masuala, je ni wa kijeshi au kidemomkrasi?

No comments: