Advertisements

Friday, May 29, 2015

Blatter anawania Urais wa FIFA


Rais wa FIFA Sepp Blatter na mpinzani wake Ali bin Hussein wa Jordan

Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter,anagombea kiti cha urais katika uchaguzi wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika leo huko Zurich Uswisi.
Uchaguzi huo unaendelea katika kongamano la kila mwaka la shirikisho hilo licha ya shinikizo kutoka kwa wadau Blatter ajiondoe kufuatia tuhuma za ufisadi na ulaji rushwa katika shirikisho hilo uliopelekea maafisa wakuu saba kukamatwa mapema juma hili.

Blatter anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mwanamfalme kutoka Jordan Ali Bin al Hussein.Jinsi kura za urais wa FIFA zilivyogawanywa.

Prince Ali Bin al Hussein ambaye matumaini yake ya kumng'oa madarakani kiongozi wa muda mrefu Sepp Blatter ilipigwa jeki hapo jana baada ya rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini kumuunga mkono.

Prince Hussein ameahidi kurejesha hadhi ya shirikisho hilo ambalo limelaumiwa kwa kuendesha magenge ya ufisadi katika uongozi wake na kura za uwezenyeji wa kombe la dunia.

Blatter tayari amekana lawama zozote dhidi yake akisema kuwa kwa kweli sio wajibu wake kuwachunga watu binafsi dhidi ya kushiriki ufisadi.Maafisa wakuu wa FIFA waliokamatwa

Blatter ambaye amepuuza shinikizo la kumtaka asiwanie urais wa FIFA anasema kuwa ni wakati wa mwanzo mpya katika FIFA.

Blatter ana ufuasi mkubwa miongoni mwa mashirika ya kandanda ya Marekani kusini Afrika na bara Asia.

Mshindi atalazimika kushinda zaidi ya theluthi mbili ya kura za wanachama zaidi ya mia mbili ilikutawazwa kuwa rais wa shirikisho hilo moja kwa moja katika mkondo wa kwanza.

Katika mkondo wa pili yeyote atakayeibuka mshindi ndiye atakaye twaa uongozi wa FIFA.

No comments: