Advertisements

Friday, May 29, 2015

WANAHABARI MKOA WA IRINGA WAKUTANA NA JESHI LA POLISI KATIKA KIKAO CHA MAHUSIANO MEMA‏

Baadhi ya wanahabari mkoa wa Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa mara baada ya kumalizika kikao chao cha mahusiano mema na kutambulishana kati ya wanahabari na viongozi wapya wa Jeshi la Polisi. Waliokaa ni Kamanda wa Polisi Ramadhan Mungi wa tatu kushoto akifuatiwa na mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard na katibu wa IPC Francis Godwin na maofisa wengine wa polisi mkoa.
Baadhi ya askari polisi wakiwa katika kikao cha pamoja na wanahabari leo.
Wanahabari wa Mkoa wa Iringa wakiwa katika kikao cha pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi.
Wanahabari wakiwa katika kikao na Jeshi la Polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa RPC Ramadhan Mungi akitoa mafunzo mafupi kwa wanahabari kati ya utendaji kazi wa jeshi la polisi na vyombo vya habari.
...akiendelea kufafanua huku wanahabari wakimsikiliza kwa makini.Wanahabari wa Mkoa wa Iringa leo wamekutana na Kamanda wa Polisi na maofisa wa jeshi la polisi mkoani hapa ili kuendelea kufanya Kazi kwa ushirikiano kwa faida ya Mkoa wa Iringa.

Katika kikao hicho kilichoambatana na semina fupi ya kukumbushana wajibu wa Kazi za wanahabari na askari.

Akitoa mafunzo hayo kamanda wa polisi wa Mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi amesema kuwa ili kuufanya Mkoa wa Iringa uweze kufanikiwa ni lazima wabahabari na polisi kufanya Kazi zao kwa kuzingatia maadili na kutofanya upendeleo katika utendaji wao.

Mungi alisema kuwa mbali ya kazi kubwa ambazo vyombo vya habari mkoani hapa vinafanywa bado jeshi lake limeamua kukutana na wanahabari hao ili kizidi kuufanya Mkoa kuwa na taswira nzuri ktk mahusiano Kati ya pande hizo mbili kama njia ya kuwatumikia wananchi.

Alisema kwa Mkoa wa Iringa vyombo vya habari vimeonyesha mchango mkubwa zaidi zaidi na kutaka mchango huo na jitihada hizo kuendelea zaidi .

Kamanda Mungi amesema kuna haja ya wanahabari na askari polisi kuendelea kujenga mahusiano kwa kukutana na viongozi wao kabla ya kufanya mapambano yasiyo na tija.

Alisema kuwa wao kama jeshi la polisi wanatambua kuwa vyombo vya habari ni muhimu kwa jamii hivyo lazima kujenga mahusiano mema na kuwa askari polisi hawanasababu ya kuendeleza mivutano

Alisema kuwa kuna wakati mwingine ajali imetokea na Kazi ya mwanahabari ni kuhabarisha umma na polisi kuokoa hivyo lazima kufanya Kazi kwa karibu na kutoa majibu stahiki kwa wanahabari na wanahabari kutotumia jazba katika utendaji Kazi zao.

Akizungumza katika mafunzo hayo mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard alisema kuwa hatua ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa kuandaa kikao hicho cha kufahamiana na mafunzo mafupi kwa wanahabari ni ya kupongezwa zaidi hasa kwa wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu.

Alisema kuwa tofauti baina ya badhi ya askari na wanahabari ilikuwa ikijitokeza kutokana na pande hizo mbili zinazofanya kazi za kijamii kutoatambuana vilivyo hivyo kila upande kuonyesha chuki dhidi ya mwingine jambo ambalo halijengi bali hubomoa.

Leonard alisema kikao hicho kina umuhimu mkubwa kwa wanahabari hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu ambao baadhi ya askari walikuwa wakiwachukia wanahabari na wanahabari kuwachukia polisi hasa kutokana na matukio ya nyuma kabla ya Mungi kuwa kamanda wa polisi wa mkoa huo wa Iringa.

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo aliomba jeshi la polisi kuwa na utaratibu wa kukutana na wanahabari japo kwa mwezi mara moja ili kujitathimini utendaji kazi wao na pale penye tofauti basi kuweza kuzimaliza kwa njia sahihi kuliko kila mmoja kutumia nguvu zisizo na tija.
Na FGBLOG

No comments: