Advertisements

Friday, April 24, 2015

Kifo Cha Msanii AK47 Taarifa Mpya Za Kushtusha Zatolewa


Ujumbe ulikuwa ukitaka Maggie amuonye mume wake AK47 aache kumfuatilia girlfriend wake anayeishi nchini Uganda anayejulikana kama Vivian Bahati.
Taarifa za Redpepper Uganda, Polisi wanaendelea kuchunguza taarifa hizo mpya, kuna Mganda ambae anaishi nchi za Scandinavia ambae anadhaniwa alikodi kikundi cha watu ambao walisababisha kifo cha AK47 kutokana na mwanamke huyo.
Polis walimpigia Maggie mke wa marehemu AK47 afike katika kituo cha Polisi cha Kabalagala kwa ajili ya kupata upande mwingine wa tukio hilo, Maggie Kiweesi alitoa vielelezo vingi ikiwemo ujumbe kutoka kutoka kwenye moja ya simu zake ambayo ilitumwa kwake kutoka kwa mtu asiyemfahamu aliyefahamika kama Sam Ssentongo.

Chanzo kimoja cha polisi kiliongeza kwamba ujumbe huo ulikuwa ukimuomba Maggie amuonye mume wake AK47 aachane na girlfriend wake aliyefahamika kwa jina la Vivian Bahati anayeishi Uganda.

Pia Maggie amewapa sauti polisi sauti ya maongezi ambayo alishafanya na Ssentongo siku za nyuma alipokuwa akimtishia kumfundisha mume somo kama hatoacha kumfuata girlfriend wake anayeitwa Vivian Bahati.

Ssengo alikuja Uganda kumtembelea mchumba wake Vivian na pia kujua ukweli kama msanii AK47 alikuwa anamfuatilia Vivian kisirisiri.

Wiki mbili baadae alisepa akiwa amechukia sana baada ya spies wake kumwambia wakiwa na uhakika na ushahidi kwamba msanii huyo alikuwa na Vivian mara nyingi kwenye gari (Bito Vox Hogen) ambayo amemnunulia.
Taarifa hizi zilipofuatiliwa polisi kujua ukweli zaidi, msemaji wa polisi Fred Enanga alisema kwamba wao kama polisi bado wajapata ushahidi uliosemwa lakini wanaendelea na kumtafuta msafishaji aliyekuwepo eneo la tukio wakati AK47 alipofariki.

“Hapa, bado sina taarifa za ushahidi mpya lakini naweza kukuhakikishia ni kwamba, akili zetu zote zinamfuatilia huyu bwana (msafishaji) amabe alishuhudia kifo cha AK47 lakini baadae alipotea kwa sababu tunadhani ndio mmoja tu anae weza kutuambia ukweli wa kilichotokea siku hiyo” Alisema msemaji huyo wa polisi Enanga.
Storri kwa mara ya kwanza ilitoka kupitia Red Pepper Uganda.

No comments: