Advertisements

Saturday, March 28, 2015

GWAJIMA AZIRAI AKIHOJIWA NA POLISI, NI KUFUATIA MANENO YA KASHFA DHIDI YA KADINALI PENGO

Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima, Josephat Gwajima, akiwa amelazwa kwenye hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam leo
Gwajima akizungumza na waandhishi wa habari alipowasili kituo kikuu cha polisi kati jijini Dar es Salaam Ijumaa Machi 27, 2015, kufuatia polisi kumtaka ajisalimishe mwenyewe
Gwajima, wakili wake, wafuasi na walinzi wake wakielekea kituo kikuu cha polisi kati Ijumaa Machi 27, 2015
Gwajima kabla ya kuzirai

Kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amezirai Ijumaa Machi 27, 2015 wakati akihojiwa na makachero wa polisi wa kituo cha kati na kulazimika kukimbizwa hospitali. Taarifa za ndani zinasema, Gwajima ambaye alijisalimisha mwenyewekituoni hapo majira ya saa nane mchana, alizirai wakati mahojiano yakiendelea majira ya usiku na ndipo polisi wakamkimbiza hospitali ya jeshi hilo Kurasini. Hata hivyo Gwajima alihamishiwa hospitali ya taifa Muhimbili kabla ya kutolewa hapo na kupelekwa hospitali ya kibinafsi ya TMJ iliyoko barabara ya Mwai Kibaki. “Hamisha hamisha” hiyo ilidumu hadi majira ya saa saba usiku na sasa kiongozi huyo wa kiroho amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu.

Gwajima ambaye anaelezwa kumiliki helikopta na magari ya kifahari, aliingia matatani baada ya mkanda wa video uluimrekodi akihutumnia mamia ya wafuasi wake kwenye viwanja vinavyotumiwa na kanisa lake, vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam wiki iliyopita akimkashifu kwa maneno makali, Askofu Mkuu wa jimbo Kuu la Dar es Salaam, kanisa Katoliki, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, kuwa hafai kuwa kiongozi wa kanisa.

Gwajima alimtuhumu Kadinali Pengo kwa kile alichokiita “kuwasaliti viongozi wenzake wa kanisa waliokubaliana kuwahamasisha waumini wao kutoipigia kura katiba pendekezi.

Hata hivyo Kadinali Pengo alipinga msimamo huo wa viongozi wenzake, na kuwataka waache kuwaamulia waumini na badala yake waumini wenyewe waachwe wajiamulie.

Habari na picha kwa hisani ya K-VIS

No comments: