Advertisements

Tuesday, January 27, 2015

‘Watakaopitishwa kugombea Urais wote wapimwe afya zao kwanza’

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, ambapo pamoja na wagombea urais alipendekeza pia na wagombea wenza kupima afya zao na majibu yao kuwa wazi ili kuepuka gharama zisizo za lazima.bwa wa nchi.

Dar es Salaam. Wagombea nafasi ya urais kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wameshauriwa kupima afya zao kabla ya kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho, ili kuepuka gharama za matibabu ya mara kwa mara za kiongozi huyo mkubwa wa nchi.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, ambapo pamoja na wagombea urais alipendekeza pia na wagombea wenza kupima afya zao na majibu yao kuwa wazi ili kuepuka gharama zisizo za lazima.

Kibamba alisema alichojifunza kwenye Uchaguzi Mkuu wa Zambia baada ya marais wawili kufariki wakiwa Ikulu na kusababisha nchi kuingia kwenye gharama za kuchagua marais mara mbili kwa kipindi cha miaka sita, kitu kilichowapa mtizamo mpya ambao ni kupima afya za wagombea urais kabla ya kuingia Ikulu.

“Suala la viongozi kupima afya hapa nchini limekuwa ni siri sana, lakini kwa mfano huu, hakuna budi viongozi kupima na kubainisha majibu ya afya zao ili kuangalia kama wanaweza kumudu mikikimikiki ya urais bila kuitia nchi gharama ya kuwatibia kila mara tena kwenye hospitali za nje, ”alisema Kibamba.

Nae Mjumbe wa Jukwaa la katiba, Islael Ilunde alisema kuwa wanaangalia uwezekanao wa kuitisha midahalo kwa wagombea ili kuwapa nafasi wananchi ya kusikia kile kinachotakiwa kufanywa na wagombea hao mara baada ya kushinda nafasi wanazozigombea.

Alisema siyo lazima kufanya mdahalo wa wagombea wa nafasi za juu , bali hata wanaogombea nafasi za kawaida wapiga kura wao wanatakiwa wafahamu kwa undani uwezo wao wa kujieleza na kupambanua mambo na ahadi zao.

“Kama vyombo vya habari na wadau wengine watashindwa kuanzisha midahalo ya kuwahoji viongozi, sisi tutazungumza na wadau wetu kuona ni kwa namna gani tutalifanya jambo hilo muhimu kwa kipindi hiki, ”alisema Ilunde.

(Mwananchi)

No comments: