Advertisements

Wednesday, January 28, 2015

Waasi Sudan Kusini wawaachia huru watoto

Wanajeshi waasi wa Sudan Kusini

Waasi nchini Sudani kusini wamewaachia huru kundi la kwanza la watoto waliokuwa wamechukuliwa kuwa wanajeshi, kundi hilo la watoto lililotegemewa kuachiwa wiki chache zijazo.

Shirika la kimataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limesema Watoto mia mbili na themanini, wengine wakiwa wadogo wa mpaka umri wa miaka 11 walikabidhiwa katika jimbo la jonglei kwa ajili ya kukutanishwa na Familia zao. Kulikuwa na furaha wakati watoto hao walipokutana na ndugu zao.

Umoja wa Mataifa unasema Wanajeshi watoto takriban 12,000 waliandikishwa katika Jeshi mwaka jana nchini Sudani kusini.

Kundi la walioachiwa ni sehemu ya Jeshi la waasi linaloongozwa na David Yau Yau ambaye alisaini mkataba wa amani na Serikali mwaka mmoja uliopita.

Mwakilishi wa UNICEF Sudani Kusini, Jonathan Veitch amesema kuachiwa huru kwa kundi hilo la watoto ni hatua ya kwanza ya matumaini.-BBC

No comments: