Advertisements

Thursday, October 30, 2014

Misa Ya Kuuaga Mwili wa Happiness Aliyekuwa Mwanachuo Wa Chuo Cha SAUT-TABORA

Jeneza lenye mwili wa Happiness aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu kishiriki cha SAUT (Archbishop Mihayo University College of Tabora - AMUCTA). Alikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika kozi ya Mahusiano ya Umma na Masoko (Public Relations and Marketing-BPRM) huku akiwa alibakisha miezi 7 tu kumaliza degree yake ya kwanza. Misa ya kuuaga mwili wa mpendwa kwa safari ya kuelekea Morogoro kwa mazishi imefanyika katika moja ya kumbi za kusomea.
Marehemu alizaliwa Tarehe 4 Juni, 1991 na kufariki tarehe 29 Oktoba, 2014 katika hospitali ya Jeshi Milambo-Tabora.


Maerehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa sickle cell na typhoid, baada ya kuzidiwa alipelekwa hospitalini siku ya jumapili hadi umauti kumkuta siku ya jana asubuhi.
Principal wa chuo (katikati) akiongoza misa ya kuuaga mwili wa marehemu Happiness W. Mhabuka
Misa ikiendelea na mwili kwenye jeneza mbele ya umati mkubwa wa wanajamii wa chuo cha AMUCTA
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Marehemu Happiness enzi za uhai wake. Kweli ni majonzi hasa.
Principal wa chuo akiongoza misa hiyo leo asubuhi katika kuuaga mwili wa mwanachuo huyo
Principal akitoa mkono wa amani kwa Scola Mhabuka (dada wa marehemu) aliyevaa kilemba cheupe na pembeni yake ni rafiki wa kiume wa marehemu Happiness.
Hatua za mwisho wa misa kuuaga mwili wa marehemu.
Mwili wa merehemu happiness ukiwa katika jeneza.
Miongoni mwa wachuo wenzake wanaosoma kozi ya PRM wakitoa heshima ya pamoja huku wakiwa na huzuni kubwa ya kumpoteza mwanachuo mwenzao happiness waliyekuwa wakimpenda lakini Mungu kafanya kazi yake isiyo na makosa.
Ni majonzi sana sana kwa kweli.
Gari iliyobeba mwili wa marehemu na kuusafirisha hadi Morogoro kwa mazishi.
Hali ya kuto amini kama kweli Happiness kawatoka bado iko akilim\ni mwa wanachuo hao wakishuhudia hadi kuondoka mwili huo. Ni masikitiko sana.
Dada wa marehemu (Kushoto) wakiongea machache na mlezi wa wanachuo madam Annah kabla msafara kuanza kuelekea Morogoro. Dada wa marehemu alifika siku ya Jumanne kwaajili ya kumuuguza na kwa bahati mbaya alifariki siku ya pili yake.
MUNGU AILAZE MAHLI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU

"Mtandao Huu Unaungana Kwa Ukaribu na Yeyote Anayeguswa na Msiba Huu"

Picha na aloyson.com

No comments: