Kushoto ni Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania,Katikati Mh:Mwigulu Nchemba Naibu katibu Mkuu CCM Bara na Kulia ni Bi,Nyeleti
Mondlane ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha FRELIMO Nchini
Msumbiji.Ujumbe huu kutoka Msumbiji ulitembea Ofisi za CCM lumbumba jana
Tar.18/09/2014 CCM
na FRELIMO ni Vyama rafiki na vyote vimeshiriki katika harakati za
Ukombozi.Hivi sasa Nchini Msumbiji wapo kwenye Kampeni za Uchaguzi Mkuu
wa RAIS,ambapo FRELIMO imemsimamisha Filipe Nyussi kuwa Mgombe
URAIS.Kihistoria Nyussi amepata kusoma Kusini mwa Tanzania mji wa
Tunduru na amepata mafunzo ya kijeshi Kambi ya Nachingwea.Naibu Katibu Mkuu CCM Bara akimvalisha skafu ya Tanzania Bi. Nyeleti Mondlane kutoka MSumbiji chama cha FRELIMONaibu
Katibu Mkuu CCM Bara Mh,Mwigulu nchemba akiwa katika picha ya Pamoja na
Ujumbe kutoka Msumbiji-FRELIMO uliofika Ofisi ndogo za Chama cha
Mapinduzi Lumumba Dsm kwaajili ya kuzingumza mambo mbalimbali ikiwamo
Uchaguzi wa Msumbiji unaotegemewa kufanyika mwaka huu.
3 comments:
Kuna jambo ambalo sherti wa-Tanzania walipambanue vizuri, muda wote. Wakati wa harakati za ukombozi Msumbiji, hapakuwa na CCM, bali TANU. Uhuru wa Mozambiki ulipatikana mwaka 1975, wakati CCM ilianzishwa mwaka 1977.
Imejengeka tabia Tanzania ya kuipa CCM maisha marefu kuliko ukweli ulivyo. Kwa mfano, ni kawaida kabisa kwa wa-Tanzania kusema kwamba CCM imekuwa madarakani miaka Zaidi ya hamsini. Inasahaulika kuwa chama kilicholeta uhuru si CCM bali TANU.
Hilo ni angalizo tu, ili tunaposoma habari kama hii ya FRELIMO na CCM tusijichanganye. Tukumbuke historia ya TANU, na tuzingatie kuwa hizo habari za CCM zinaanzia mwaka 1977.
MDAU NAKUUNGA MKONO SANA KATIKA HILI SABABU MIMI 1974 NILIIMBA SANA NYIMBO ZA UKOMBOZI KUHUSU ZIMBZBWE,MOZAMBIQUE,SOUTH AFRICA NA NAMIBIA.WAKATI HUO NILIKUWA TYL yaani TANU Youth Leage. TANU ndilo chama la ukombozi. Labda hawa watu waZANU PF hao walipiganiwa pia na CCM. Watanzania tujue jinsi ya kupambanua civics na historia kimaandishi
Tanu CCM ndiyo wale wale tu. Ni jina tu limebadirika. Watu na itikadi ni zilezile. To me if I blame ccm then I blame Tanu too. If I praise Tanu I praise ccm on the other hand. Viongozi wote wakuu wa Tanu si ndiyo walio ingia ccm? Sasa angalizo lipi tena unaweka? Tofauti ni majina tu dada hakuna kingine.
Post a Comment