Advertisements

Tuesday, July 29, 2014

RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA AZUNGUMZA NA VIONGOZI VIJANA TOKA BARANI AFRIKA

Ukumbi wa Regency Ballroom katika Hotel ya Omni Shoreham Washington DC ukiwa umepambwa kwa Bendera toka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry akitoa hotuba yake kwa Viongozi vijana toka barani Afrika waliokuwa wakishiriki mafunzo katika vyuo vikuu vya Arkansas na Florida nchini Marekani.
Rais wa Marekani ,Barack Obama akizungumza na Viongozi vijana toka nchi mbalimbali za Afrika waliokuwa wakipata mafunzo katika vyuo vikuu vya Arkansas na Florida.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari ni miongoni mwa Vongozi vijana toka barani Afrika waliohudhuria mkutano huo na Rais Barack Obama hapa akifuatilia kwa makini Hotuba ya Rais Obama.
Mbunge Joshua Nassari akiwa na Viongozi vijana wenzake walioshiriki mafunzo hayo nchini Marekani.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akionesha cheti chake cha kuhitimu mafunzo ya wiki tisa yaliyoshirikisha Vongozi vijana toka barani Afrika .
Cheti cha kuhitimu Mafunzo ya wiki tisa alichotunukiwa Mbunge Joshua Nassari baada ya kuhitimu mafunzo ya wiki tisa yaliyoshirikisha Viongozi Vijana nchini Marekani

1 comment:

baraka daudi said...

Hongera sana mbunge wetu Mheshimiwa Joshua Nassari. Hii inatia moyo sana kwa vijana kuona Mheshimiwa anatuwakilisha vizuri. Tafadhali ulichojifunza katika semina hiyo uwapeleke na kulitumikia Taifa letu. Nakutakia kila la heri na mafanikio makubwa katika ujenzi wa Taifa letu.