Advertisements

Wednesday, April 23, 2014

WAZIRI MKUU SPORTS CLUB YAANZA KWA KISHINDO MASHINDANO YA MEI MOSI, MOROGORO

Wanamichezo wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaoshiriki katika Mashindano ya Mei Mosi Mjini Morogoro, wakipita mbele ya mgeni Rasmi, Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Joel Bendera (hayupo pichani) wakati wa Ufunguzi wa mashindano hayo jana. Washiriki wa Mashindano hayo ni Wizara, Idara na Taasisi za Serikali zinazojitegemea.Kikosi kabambe cha Mpira wa miguu cha Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshiriki katika Mashindano ya Mei mosi yanayoendelea mjini Morogoro.
Timu ya kamba ya wanawake ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakivutana na Timu ya Alliance One ambapo Timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu imeshinda katika mchezo huo.
Timu ya kamba Wanaume ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakivutana na Timu ya Alliance One ambapo Timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu imeshinda katika mchezo huo. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

No comments: