Advertisements

Tuesday, April 22, 2014

TAARIFA KUHUSU JURGEN KLOPP KUCHUKUA MIKOBA YA DAVID MOYES

jurgen klopp
Jürgen Klopp amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kuteuliwa nafasi ya ukocha wa klabu ya Manchester United. Kocha huyo mwenye miaka 46 ameliambia gazeti la The Guardian la Uingereza: “Man Utd ni klabu kubwa na nahisi kuwa mazingira yake nina uzoefu nayo na ina mashabiki wazuri sana, lakini mpaka sasa nina mkataba na Dortmund na imani yangu kwa mashabiki wa klabu hiyo haiwezi kuvunjwa.”
Klopp, ambaye anatajwa kuwa na kipenzi kikubwa cha bodi ya wakurugenzi ya Manchester United, aliongeza mkataba wake na Dortmund mpaka 2018 mwaka jana Oktoba na alikaririwa akisema kwamba bado anaipenda klabu hiyo wiki iliyopita. Inaaminika United walijaribu kufanya mazungumzo na Dortmund lakini walijibiwa kwamba Klopp hakuwa na nia ya kuvunja mkataba wake ndani ya Signal Iduna Park.

No comments: