Advertisements

Thursday, April 17, 2014

BREAKING NEWZZ!!N/WAZIRI WA FEDHA MWIGULU NCHEMBA AFUTA MALIPO,AZUIA BENKI KUWALIPA WALIOTOROKA BUNGENI "UKAWA"

 
Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Lameck Nchemba
Ikiwa ni Siku ya pili tangu Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo,Cuf na NCCR Mageuzi wanaounda kitu kinachoitwa UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai wamechoka Kutukana na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa Waziri wa
Fedha tangu Tarehe.10./04/2014 hadi 18/04/2014 kutokana na Waziri wa Fedha kusafiri Nchini Marekani Kikazi,amefuta Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato wa Katiba.
Habari za Uhakika Kutoka Chanzo chetu ndani ya hazina kinasema,Mwigulu Nchemba ameagiza Mabenki yote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating allowance zilizopelekwa na Bunge jana tar.16/04/2014 ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka tar.30/04/2014.Pia ilikujiridhisha na taarifa hizo,Mwandishi wetu alizungumza na Wajumbe namna Mtiririko wa Malipo unavyofanyika ndani ya Bunge hilo,Mjumbe(Jina tunalihifadhi) alisema fedha zote zinapitia Benki na wakati wanajiandikisha siku za Kwanza walitakiwa Kuandika namba zao za Benki na Malipo yote hupitia huko,hivyo kama ni fedha zinazuiliwa Benki.

Baadhi ya wabunge wa CUF na Chadema wanaojiita UKAWA toka jana walijua wameshasaini fedha hizo hivyo zitaingia kwenye account zao Binafsi. Mambo yamekuwa tofauti baada ya Naibu Waziri wa Fedha(Sera) Mh:Mwigulu  kuagiza leo form zisainiwe upya leo na zitasainiwa pia tar 22 mpaka 25,Kwa madai ya asiyefanya kazi na asile. 
Mbali na hilo,Mh:Mwigulu amenukuliwa na clouds fm akisisitiza Rais kuwafuta wajumbe wakiojitoa na badala yake awateue watu waliotayari kutunga katiba hata bure kuliko hawa wanaokutana vikao lukuki kupanga njama za kususia mchakato. Aidha Mwigulu alisema fedha inayotumika ingeweza kulipwa Wazabuni wanaozidai halmshauri, wangeweza kulipa madeni ya walimu, au kuwapa mikopo watoto wa masikini waliofaulu ila hawajaenda vyuo kwa kukosa mikopo, au zingenunua madawa hosipitalini, au zingepeleka umeme, maji, vitabu au barabara lakini wamelipwa wajumbe badala ya kufanya kazi hiyo wanapanga njama ya kuhujumu mchakato usiendelee kwa kutafuta visingizio lukuki.
Bunge la Katiba linategemewa kuendelea Tar.22 Mwezi huu mara baada ya sikukuu za Pasaka Kupita na litaahirishwa tena Tar 25 mwezi huu kupisha Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

5 comments:

Anonymous said...


Wrong politics/leadership! Mwigulu ambaye alisimama bungeni kuwasema vibaya ukawa, leo ametumia cheo chake serikalini kuzuia malipo yao? Ni sawa asiyefanya kazi asile lakini hii itasababisha chuki binafsi zaidi. Ni bora naibu mwingine wa wizara ya fedha angechukua hatua hiyo kwa niaba ya waziri. Na kwani waziri akiwa Marekani hawezi kuchukua hatua hiyo wakati huu wa mtandao?

Anonymous said...

jamani huyu hata sijui shule gani kaenda yani nimeangalia interview zake anavyozungumza nimeona sifuri sifuri tuu nimemchunguza kadogo longtime tu tuka apate wazifa huu nimegundua kweli bongo mambo yote shagala baglaaa si siri ukijua channels mambo waaa

Anonymous said...

Huu ni usanii wa Kisiasa tu, hakuna cha kutetea mtu mnyonge hapa. Laiti kama serikali ingekuwa na uharaka kama huu wa kuzuia na kurejesha mabilioni ya fedha kutafunwa na mafisadi kama zile za EPPA au zinazolipwa kwa makndarasi hewa pamoja na ufujaji mkubwa kwenye halmashauri za wilaya na miji! Hivi serikali imekuwa wapi siku zote (miaka 50) kutoa hizo huduma za msingi kwa jamiiya Watanzania ambazo Mh. Kaimu Waziri wa Fedha anasema zingelipwa na posho ya hawa wajumbe waliosusia kikao cha kujadili (kupeana mipasho kuhusu) Katiba Mpya? Jamani tuache siasa za maji taka, tuwe serious na maisha ya wanainchi wengi wanaoteseka huko vijijini.

Anonymous said...

I am not fan of Hon Nchemba (because of his brainless contributions in the parliament and his irrelevant hojas which a waste of time BUT I support him on this. Tanzania has limited resources. Some wananchi lost their houses and belongings because of the recent floods. Instead of paying UKAWA let the money restore some loss caused by floods.

Anonymous said...

Well kwenda bungeni is part of work now kusimamisha kulipwa is a start but wale walioiba pia wachukuliwe hatua na warudishe pesa zote even mali zao zichukulir na kuuzwa ili pesa irudi na wao weende jela....upuuzi why waziri mwenyewe hakufanya hivyo ...yani ujinga daily. .bunge la sasa ni kama sokoni kariako kila muuza nyanya apiga kelele so are these wabunge waongo na wachama kimoja kinachotawala