Advertisements

Sunday, May 1, 2016

DKT. SHEIN KATIKA SHEREHE ZA SIKU YA KILELE CHA WAFANYAKAZI DUNIANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi, wakipita mbele yake wakati wa sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi,(pichani) Vijana waliobeba bango kutoka Ofisi ya Makamo wa Pili ya Rais akipita mbele yake wakati wa sherehe za sikuya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.

DICOTA 2016 DALLAS, TEXAS SIKU YA MWISHO YA KONGAMANO

Balozi wa Tanzania akifuatilia kongamano la DICOTA 2016 lililofikia ukingoni siku ya Jumamosi April 2016 jijini Dallas, Texas nchini Marekani. Picha na Vijimambo/Kwanza production
Wawakilishi wa CRDB wakifuatilia kongamano.
Mwakilishi wa CRDB
Wadau mbalimbali kutoka majimbo tofauti wakifuatilia kongamano

RAIS MAGUFULI ASHUSHA KODI YA MAPATO YA MSHAHARA (PAYE) KUTOKA ASILIMIA 11 HADI 9

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli  ametangaza kushusha kodi ya mapato ya Mshahara ( Pay as you Earn -PAYE  )  kutoka asilimia 11 iliyopo sasa hadi asilimia 9.

Rais amesema ameamua kuchukua umamuzi huo ili kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni ya kuwapunguzia mizigo wafanyakazi kwa kuwaongezea mishahara na kuwapunguzia kodi ya mapato ya mishahara.

Kuhusu kuwaongezea mishahara, Rais Magufuli ameomba wafanyakazi wamvumilie kwa kuwa hivi sasa yuko kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuziba mianya yote ya Rushwa.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amewataka waajiri wote nchini kuwapa wafanyakazi wao mikataba ya ajira na kupeleka makato yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii bila kukosa

YANGA YAANGUKIA PUA, YACHAPWA 3-1 NA SIMBA UGHAIBUNI, RENATUS NJOHOLE ATUPIA 1, NICO USIPIME

Wachezaji wa Simba wakisimama kwa dakika moja kwa ajili ya misiba iliyotokea Houston, Texas kwa Watanzania Henry Kiherile na Andrew Sanga waliopoteza maisha kwa ajali ya kupigwa  risasi. Picha na Vijimambo/Kwanza Production.
Wachezaji wa Yanga wakisimama kwa dakika moja kwa ajili ya misiba iliyotokea Houston, Texas kwa Watanzania Henry Kiherile na Andrew Sanga waliopoteza maisha kwa ajali ya kupigwa  risasi

Mchezaji Renatus Njohole akiwatoka mabeki wa Yanga.
Mke wa Balozi Marystela Masilingi akiwa uwanjani kuishabikia Simba.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akikabidhi kombe kwa nahodha wa Simba Bagasa
Mhe. Balozi Wilson Masilingi na mkewe Marystela Masilingi wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Simba walioibamiza Yanga kwa bao 3-1 mechi iliyoanaliwa na DICOTA 2016 Dallas Texas.
Kikosi cha Simba Ughaibuni
Kokosi cha Yanga Ughaibuni.
Timu ya Simba iliendeleza ubabe kwa mara ya nne mfululizo nje ya DC baada ya jana Jumamosi April 30, 2016 kuibanjua timu ya Yanga bao 3-1 katika mechi iliyoandaliwa na kongamano la DICOTA 2016 lililomalizika siku ya Juamamosi jijini Dallas, Texas nchini Marekani.

Wanandugu wawili Nico Njohole na Renatus Njohole waliowahi kuichezea Simba ya jijini Dar es Salaam na timu ya Taifa kwa nyakati tofauti, walikua kizingiti kikubwa kwa Yanga ambao jana waliuanza mchezo kwa kasi na kupata bao la kuongoza kupitia mchezaji wao hatari Dulla Makubeli.

Baada ya bao hilo Simba ilitulia na kucheza soka la kitabuni huku ikiongozwa na wakongwe wawili ambao walicheza soka lililowashangaza wengi lililosaidia Simba kusawazisha bao safi katika dakika 44 ya kipindi cha kwanza kupitia mchezaji James Kitia. Bao hilo lillisababishwa na mchezaji Renatus Njohole baada ya kuambaa na mpira wingi ya kushoto na kutia krosi iliyomkuta James Kitia na kufunga goli zuri la kideo kwa kichwa,

Kichupa cha leo Nasi Ft Shaa - Nikilewa (Official Video)

VIJIMAMBO INAKUTAKIA JUMAPILI NJEMA NA JANET OTIENO-TEMBEA NAMI

Serikali Yaokoa Sh. Bilioni 15.4 za Mishahara HEWA Machi hadi Aprili 24

Serikali imetangaza kuokoa kiasi cha Sh15.4 bilioni katika kipindi cha kuanzia Machi hadi Aprili 24 ambacho kingelipwa kwa watumishi hewa 8,236 ambao wamebainika hadi sasa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Angela Kairuki aliliambia Bunge jana kuwa kazi ya kuwasaka watumishi hewa bado inaendelea nchini kote.

Alisema watumishi hao wamebainika katika maeneo mbalimbali na kati yao 1,614 ni wa Serikali Kuu na 6,624 wa Serikali za Mitaa.

Waziri alisema kuwapo kwa watumishi hewa kumewafukuzisha kazi maofisa 56 na taratibu za kuwafungulia kesi mahakamani zinaendelea ikiwamo kutakiwa kulipa hasara yote ambayo waliisababisha.

WAFUNGWA WANAOSUBIRI KUNYONGWA MAGEREZANI WAFIKIA 465

IDADI ya Watanzania wanaosubiri kunyongwa imekuwa ikiongezeka na hadi sasa imefikia 465 kutokana na hukumu ya kifo kutotekelezwa tangu mwaka 1994. 

Ripoti iliyotolewa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika mafunzo kwa waandishi wa habari mjini Morogoro juzi, imebainisha kuwa hakuna hukumu yoyote ya kifo iliyosainiwa na Rais ili kutekelezwa hadi Oktoba 2015 kulipofanyika Uchaguzi Mkuu ambao Rais Magufuli aliibuka mshindi.

Ripoti hiyo ya Mpango wa Kujitathmini Kuhusu Hali ya Utekelezaji wa Haki za Binadamu (UPR), unaotekelezwa kwa mara ya pili nchini, imeonesha kuwa kuna mahabusu 465 wanaosubiri adhabu ya kifo, kati yao wanaume ni 445 na wanawake ni 20.

Wanaharakati 
Akiwasilisha ripoti hiyo, Ofisa Uchunguzi Mkuu wa Tume hiyo, Philemon Mponezya, alisema Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, inaitaka Serikali kufuta adhabu hiyo kwa kuwa haitekelezeki lakini baadhi ya asasi hasa zinazohusika na haki za walemavu wa ngozi, zinapinga kufutwa kwa adhabu hiyo.

Waziri Mhagama atoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (kulia) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 na jinsi dawa hizo zinavyoathiri afya na nguvu kazi ya taifa. Kushoto ni Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya nchini Keneth Kiseke.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (kushoto) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 na jinsi dawa hizo zinavyoathiri afya na nguvu kazi ya taifa. Kulia ni Mfamasia Sehemu Elimu, Habari na Takwimu Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya nchini Amani Masami.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma)

WABUNGE WA CCM WAKATAA BUNGE KUONYESHWA LIVE, WAPINZANI WAAMUA KUJIREKODI KWA SIMU ZAO

Wabunge wa CCM jana waliibuka kidedea walipowazidi wenzao wa upinzani kwa kura za sauti “Siyooooo” kuikataa hoja ya kutaka matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja ‘live’ na televisheni. 

Hiyo ilitokea jana wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ya Ofisi ya Rais (Tamisemi na Utumishi na Utawala Bora) na kuzua mvutano mkali uliosababisha bajeti hiyo ipitishwe kwa utaratibu wa wabunge kutohoji kitu chochote (guillotine).

Wakati hoja yao hiyo ikipingwa kila kona, tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti, wabunge hao wa upinzani sasa wamebuni mbinu mpya ya kujirekodi wenyewe wakati wakichangia mijadala mbalimbali bungeni na kurusha sauti zao kwenye mitandao ya kijamii na kupeleka sauti hizo kwenye redio zilizopo katika maeneo ya majimbo yao.

ATUPWA JELA MIAKA 12 BAADA YA KUJIFANYA OFISA USALAMA WA JK

Mahakama ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, imemhukumu kwenda jela miaka 12, Qasama Machibya aliyejifanya ofisa usalama wa Taifa kwenye ziara ya Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete mwaka 2013.
Kabla ya hukumu, mshtakiwa alijitetea mahakamani hapo kuwa kitambulisho alichokutwa nacho siyo chake na anashangaa kuona kuna picha yake na jina lake.
Alidai kuwa hizo ni mbinu za polisi kumminya, hivyo aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu na kwamba ana ugonjwa wa Ukimwi.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Gabriel Kurwijila alisema utetezi wa mshtakiwa hauifanyi mahakama kutomtia hatiani kwa kuwa hana cheti cha ugonjwa.
Alisema kutokana na mahakama kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka uliowasilishwa inamtia hatiani kwa makosa matatu.
Kurwijila alisema kosa la kwanza ni kughushi nyaraka ya Serikali hivyo, atakwenda jela miaka mitano na kosa la pili la kujifanya

DIWANI AMSHAMBULIA MWENZAKE KWA CHUPA

Diwani wa Kata ya Maparoni, Haji Ngachoka (CUF) ameshambuliwa kwa kupigwa na chupa ya maji na diwani wa Viti Maalumu, Amina Mapande (CCM) katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kikiendelea wilayani hapa leo.
Tukio hilo lilitokea wakati Ngachoka alipokuwa akitoa hoja ya kupinga mgawanyo wa mipaka ya wilaya mpya ya Kibiti kuwa ipakane ndani ya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, wakati kijiografia ipo ndani ya Jimbo la Rufiji.
Akizungumzia tukio hilo, Ngachoka alidai alikuwa akitoa hoja, ndipo aliposhtuka akipigwa chupa ya maji usoni na diwani huyo bila kujua sababu za kupigwa kwake.
“Nilikuwa nikitoa hoja ya kupinga mipaka ya Wilaya mpya ya Kibiti ipakane na Wilaya ya Kilwa, ghafla nilishtukia nimepigwa na chupa ya maji usoni na Amina, baada ya tukio hilo alikuwa akijiandaa kunipiga tena na chupa ya soda ikadakwa,” alidai.

MAGAZETI YA LEO MAY 01, 2016

TUME YA PAMOJA KUFUATILIA ZIARA YA RAIS MAGUFULI NCHINI RWANDA

Kikao cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda kilichofanyika kuanzia tarehe 29 – 30 Aprili, 2016, kimekamilika Mjini Gisenyi, Rwanda, ambapo wataalam wa sekta mbalimbali wameazimia kuharakisha maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. 
 
Kikao hicho cha 14 cha ushirikiano kimefanyika kufuatia maagizo ya Marais wa Tanzania na Rwanda wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli nchini Rwanda mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu. 
 
Wakati wa ziara hiyo, wakuu hao walikubaliana kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano na kuibua maeneo mapya yanayolenga kuinua shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.

Saturday, April 30, 2016

MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA AONGOZA KAMPENI YA USAFI JIJI LA DAR LEO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na Naseeb Abdul "Diamond Platnumz " Simba , Ruge Mutahaba wa Clouds Fm na wengine wengi wakishiriki Kampeni ya Usafi Leo Dar ya Makonda 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakiongoza maelfu ya Wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika matembezi maalum ya kampeni ya kuhamashisha usafi katika jiji hili #Dar es salaam Ya Makonda, Usijifanye Mstaarabu kuwa Mstaarabu. Karume, Ilala na kuishia katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.

DKT. SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI KATIKA TAASISI MBALI MBALI ZANZIBAR LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Salmin Amour Abdalla kuwa Naibu Katibu wa Baraza la Mapinduzi katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Asaa Ahmada Rashid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.

JENGO LENYE GHOLOFA SITA LAPOROMOKA NA KUUA WATU SABA NAIROBI

Polisi katika mji mkuu wa Kenya Nairobi wanasema kuwa takriban watu saba waliuawa wakati nyumba moja ilipoanguka katika mtaa mmoja mjini humo. Waokoaji wanaendelea kutafuta watu wanaohofiwa kukwama ndani ya vifusi vya jengo hilo la ghorofa sita kufuatia mvua kali inayoendelea kunyesha ambayo imesababisha mafuriko.
Takriban watu 120 wameokolewa kufikia sasa katika mtaa huo wa Huruma. Shirika la msalaba mwekundu linasema kuwa takriban familia 150 ziliathiriwa na mkasa wa jumba hilo lililojengwa miaka miwili iliopita Waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali ya Mama Lucy iliopo mjini humo.

AJALI YAUA WATU WATANO MKOANI MBEYA

Watu watano wamefariki dunia na wengine 29 kujeruhiwa katika ajali ya basi la HBS eneo la Maji Mazuri, Mbeya Vijijini.
Basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya mjini kuelekea Tabora kuitia Chunya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala aliyekuwa kwenye shughuli za kusimamia usafi ameenda kwenda eneo la tukio ili kusaidia uokoaji.
Akizungumza baada ya kutoka eneo la tukio, amesema waliofariki dunia ni wanaume wawili na wanawake wawili na mtoto mdogo, ambao bado majina yao hayajatambuliwa na majeruhi ni 29.
Taarifa za awali inadaiwa ajali hiyo imesababishwa na gari kufeli breki na kisha kugonga gema na kupinduka. Dereva aliruka na kutokomea kusikojulikana.

MAPENDEKEZO YA SHERIA YA WAZEE KUWASILISHWA BUNGENI

NAIBU WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali imekamilisha mapendekezo ya uundwaji wa Sheria ya Wazee ambayo yatawasilishwa katika mkutano wa Bunge wa Septemba.

Dk. Kigwangalla aliyasema hayo jana (Ijumaa, Aprili 29, 2016) wakati akitoa ufafanuzi kwa Viongozi wa Mtandao wa Wazee waliomtembelea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake mjini Dodoma.

Dk. Kigwangalla alisema kuwepo kwa Sheria ya Wazee kutawezesha mambo mbalimbali yanayohusu wazee kutekelezwa kwa mujibu wa sheria hiyo likiwemo suala la pensheni.

Mkutano wa Kiroho - Columbus, OhioNICO NJOHOLE NA RENATUS NJOHOLE KUONGOZA SIMBA UGHAIBUNI, MPAMBANO WA WATANI WA JADI DALLAS, TEXAS LEO


Kikosi cha Yanga ughaibuni
Kikosi cha Simba ughaibuni
Renatusi Njohole akiwa katika picha ya Nico Njohole Dallas, Texas.

Wanandugu wawili Nicodemus Njohole na Renatus Njohole ambao kwenye nyakati tofauti waliwahi kuchezea timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi April 30, 2016 wataiongoza timu ya Simba ughaibuni kwenye mpambano wa watani wa jadi utakaofanyika jijini Dallas, Texas nchini Marekani.

Hii itakua ni mara ya nne kwa mpambano huu wa Simba na Yanga kuchezwa nje ya DC. Kama ilivyozoeleka watani hawa wa jadi mara nyingi mechi zao hufanyikia Washington, DC, na mara zote Yanga inaibuka mshindi.

Majimbo mengi ambako mpambano huu ulishawahi fanyika ni Columbus, Ohio, Chacago, Illinois na Houston, Texas.